#HABARI: Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Afya, Dkt. Jafar Seif, amesema anakusudia kuzunguka nchi nzima kuzungumza na watumishi wa kada ya afya ngazi ya msingi ili kusikiliza changamoto zao na kujadiliana kwa pamoja juu ya namna bora ya utatuzi wa changamoto hizo, ikiwa ni sehemu ya kwanza ya uboreshaji wa huduma za afya nchini kuelekea mpango wa bima ya afya kwa wote.

Naibu Waziri, Dkt. Seif, ameyasema hayo wakati akizungumza na watendaji wa Hospitali ya Wilaya ya Makete mkoani Njombe alipofanya ziara ya ukaguzi wa mwenendo wa maboresho ya miundombinu na kukagua vifaa tiba vya kisasa vilivyonunuliwa na Serikali ya Awamu ya Sita kwa lengo la kusogeza huduma za kibingwa karibu na wananchi katika maeneo ya pembezoni mwa miji.

Awali, Katibu wa Afya wa Hospitali ya Wilaya ya Makete Aderiko Dominick amempongeza Naibu Waziri Dkt. Seif kwa namna alivyotoa nafasi ya kusikiliza changamoto za watumishi wa kada ya afya na kada zingine katika wilaya ya Makete, akipongeza kile alichodai kuwa ni busara katika kuzungumza na watumishi wanaohudumu katika maeneo ya pembezoni ambayo kwa namna moja au nyingine yanakabiliwa na changamoto za kimazingira.

‎Powered by #MCHEZOSUPA

‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *