Wananchi wanaosafiri kati ya Kigamboni na maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam wamesema kuwa huduma za Azam Sea Taxi zimewarahisishia maisha kwa kupunguza muda mrefu waliokuwa wakiutumia kusubiri vivuko.
Wamesema huduma hizi si tu zinafanya usafirishaji kuwa rahisi, bali pia zinaboresha ufanisi wa shughuli zao za kila siku, kwani sasa wanaweza kupanga muda wao vizuri.
#AzamTVUpdates
✍Ibrahim Kilumbo
Mhariri | John Mbalamwezi