Wizara ya Usalama ya Iran imetangaza kuwa imewatia nguvuni mamluki wawili wenye mfungamano na kundi la kigaidi la Munafiqin (MKO). Mamluki hao walikuwa wapiongozwa na kupewa maagizo la uongozi wa kundi hilo wenye makao yake nchini Ujerumani.

Wizara ya Usalama ya Iran imeeleza kuwa mamluki hao wawili waliokamatwa walikuwa na nyumba wakiitumia kama maficho yao hapa Tehran. Kulingana na hati zilizokamatwa na kukiri kwa mamluki hao, uongozi wa kundi la Munafiqin nchini Ujerumani lilifanua jukumu la vibaraka wanaowatumia kuwa ni kuichoma moto misikiti na kuwachinja watu.

Mamluki hao wa ugaidi waliokamatwa na Wizara ya Usalama ya Iran wamesema kuwa uongozi wa kundi la Munafiqin nchini Ujerumani uliwahamishia kiasi kikubwa cha fedha kwa njia ya siri kwa ajili ya kununua silaha, kupata nyumba salama ya kuishi, na mahitaji mengine kwa ajili ya kuendesha uhalifu wa kutumia silaha. 

Maafisa wa Wizara ya Usalama ya Iran wameeleza kuwa silaha baridi kadhaa, bunduki mbili aina ya Kalashnikov zenye risasi, na vifaa maalumu vya mawasiliano vilinaswa kutoka kwa washukiwa hao.

Katika oparesheni nyingine, vikosi vya usalama vya Iran vimeinasa timu ya kigaidi iliyokuwa imejipenyenza nchini ikitokea katika mipaka ya magharibi mwa Iran kwa shabaha ya kutekeleza mauaji na uharibifu katika ghasia za karibuni. 

Timu hiyo ya magaidi ilihusika katika shambulio la kutumia silaha dhidi ya kituo cha polisi nambari 126 katika eneo la Tehran Pars mashariki mwa Tehran jioni ya Januari 8 mwaka huu. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *