Mgombea urais wa chama cha upinzani nchini Tanzania ACT Wazalendo, Luhaga Mpina, sasa anakabiliwa na pingamizi jingine la kisheria kama mgombea, baada ya mwanasheria wa serikali na vyama vingine viwili vidogo vya upinzani, kuwasilisha mapingamizi mapya dhidi yake, chama chake kimethibitisha.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mapingamizi haya mapya dhidi ya Mpina, yanakuja siku chache kupita tangu mahakama kuu itoe uamuzi kuagiza arejeshwe katika mchakato wa uchaguzi, mapingamizi haya mapya yakitishia kampeni zake wiki chache kabla ya uchaguzi wa Oktoba 29.

Kwa mujibu wa chama chake, waliowasilisha mapingamizi ni pamoja na ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali pamoja na wagombea wa vyama vya AAFP na NRA, wote wakipinga mchakato wa chama chake uliotumika kumteua kugombea urais.

Katika taarifa yake, ACT imekosoa mapingamizi hayo, ikisema yanalengo la makusudi kukwamisha kampeni zake, ambapo imekituhumu chama tawala CCM kuwa nyuma ya mpango huu, chama hicho sasa na chenyewe kikisema kitamuwekea pingamizi Samia Suluhu Hassan.

Mapingamizi haya yanakuja wakati huu baadhi ya wadau wandani na nje ya nchi hiyo, wakiwa na wasiwasi kuhusu uelekeo wa hali ya demokrasia, wakati huu pia chama kikuu cha upinzani CHADEMA kikisusia uchaguzi wa mwaka huu, ambapo pia mwenyekiti Wake Tundu Lissu akisota rumande kwa tuhuma za uhaini.

Aidha hivi leo, mahakama kuu ya Dar es Salaam, inatarajiwa kutoa uamuzi mdogo wa mapingamizi yaliyowasilishwa na Tundu Lissu, ambaye anataka aachiwe huru kwa kile amedai kutotendewa haki katika mahakama ya awali iliyosikiliza mchakato wa kuthibitisha mashtaka dhidi yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *