
Vikosi vya Israel vimeharibu takriban majengo 30 ya makazi huko Gaza na kuwalazimisha maelfu ya watu kuhama makazi yao, maafisa wa Palestina wamesema, wakati Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio akiwasili siku ya Jumapili kujadili mustakabali wa mzozo huo.
Imechapishwa:
Dakika 3 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Israel imetangaza azma yake ya kuuteka mji huo ambapo takriban Wapalestina milioni moja wamekimbilia, ikiwa ni sehemu ya lengo lake lililotajwa la kulitokomeza kundi la wanamgambo wa Hamas, na kuzidisha mashambulizi yake kwa kile inachokiona kuwa ngome ya mwisho ya kundi la wanamgambo hao wa Palestina.
Uongozi wa kisiasa wa Hamas, uliokuwa katika mazungumzo ya hapa na pale juu ya uwezekano wa kusitisha mapigano na makubaliano ya kuwaachilia mateka, ulikuwa lengo la shambulio la anga la Israel huko Doha siku ya Jumanne, shambulio lililolaaniwa vikali.
Qatar itakuwa mwenyeji wa mkutano wa dharura wa kilele wa mataifa ya Kiarabu na Kiislamu leo Jumatatu kujadili hatua zinazofuata. Rubio amesema Washington imetaka kujadili kuachiliwa kwa mateka 48 ambao bado wanashikiliwa na Hamas katika Ukanda wa Gaza na ujenzi wa ukanda wa pwani. Ni 20 tu kati yao wanaoaminika kuwa bado wako hai. “Kilichotokea kimetokea,” amesema. “Tutakutana nao (viongozi wa Israel). Tutajadili mustakabali wa mzozo huo,” Rubio alisema kabla ya kusafiri kwenda Israel, ambako atasalia hadi Jumanne.
Mara baada ya hapo, Rubio alizuru eneo la maombi ya Kiyahudi kwenye Ukuta wa Magharibi huko Jerusalemu. Atakutana na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.
Ziara ya Ukuta wa Magharibi ilikusudiwa “kuthibitisha tena utambuzi wa Marekani kwa Jerusalemu kama mji mkuu wa milele wa Israel,” kulingana na taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje.
Mwishoni mwa mwaka 2017, wakati wa muhula wake wa kwanza kama rais, Donald Trump alitambua rasmi Jerusalem kama mji mkuu wa Israel na baadaye kuhamisha Ubalozi wa Marekani kutoka Tel Aviv kwenda Jerusalemu. Philippe Lazzarini, Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi wa Kipalestina katika Mashariki ya Karibu (UNRWA), amesema katika ujumbe uliochapishwa kwenye mtandao wa kijamii wa X siku ya Jumapili kwamba shirika hilo limesitisha huduma katika kliniki ya Beach Camp, ambayo amesema ndiyo kituo pekee cha afya kinachopatikana kaskazini mwa Wadi Gaza. Huduma za maji na usafi wa mazingira sasa ziko katika nusu ya uwezo wake, Lazzarini amesema, akiongeza kuwa majengo 10 ya UNRWA yameathirika katika Jiji la Gaza katika muda wa siku nne zilizopita.
Mkataba wa Abraham hatarini
Maafisa wa Marekani wametaja shambulio la siku ya Jumanne dhidi ya wajumbe wa Hamas nchini Qatar, mshirika wa karibu wa Marekani, kuwa ni ongezeko la mzozo la upande mmoja ambalo halikusaidia maslahi ya Marekani wala Israel. Rubio na Rais Trump wa Marekani wote walikutana na Waziri Mkuu wa Qatar Mohammed bin Abdulrahman al-Thani siku ya Ijumaa.
Netanyahu alitia saini makubaliano Alhamisi ya kuendeleza mpango wa upanuzi wa makaazi ambayo yatapitia Ukingo wa Magharibi, eneo ambalo Wapalestina wanadai kuwa kuwa litakuwa jimbo la taifa hilo la baadae. Hatua hiyo, kwa mujibu wa Umoja wa Falme za Kiarabu, itahatarisha Mkataba wa Abraham ulioidhinishwa na Marekani, ambao ulifufua uhusiano kati ya Imarati na Israel.
Mashirika ya misaada yanasema kuwa kama Israel itatwaa mji wa Gaza itakuwa janga kwa wakazi ambao tayari wanakabiliwa na utapiamlo. Wapalestina wengine wawili walikufa kutokana na utapiamlo na njaa huko Gaza katika muda wa saa 24 zilizopita, wizara ya afya ya eneo hilo imesema siku ya Jumapili, na kufanya idadi ya vifo kufikia 422, wakiwemo watoto 145.
Israel, ambayo ilizuia chakula chochote kuingia Gaza kwa wiki 11 mapema mwaka huu, imekuwa ikiruhusu msaada wa ziada katika eneo hilo tangu mwishoni mwa mwezi wa Julai ili kuzuia uhaba zaidi wa chakula, ingawa Umoja wa Mataifa unabaini kwamba kiasi kikubwa zaidi kinahitajika. Israel inasema inataka raia kuondoka katika mji wa Gaza kabla ya kutuma vikosi vya vinginz vya ardhini. Makumi ya maelfu wanakadiriwa kuondoka katika Jiji la Gaza, lakini mamia ya maelfu wamesalia katika eneo hilo. Hamas imewataka raia kubaki katika Jiji hilo.
Vikosi vya Israel vimekuwa vikifanya kazi kwa wiki kadhaa katika angalau vitongoji vinne vya mashariki, na kugeuza angalau vitatu kuwa maeneo yasiyo kuwa na watu. Jeshi la Israel linakaribia katikati na magharibi mwa eneo hilo, ambapo wengi wa waliokimbia makazi yao wametafuta hifadhi. Wengi wa watu hawa wanasitasita kuondoka, wakisema hakuna nafasi au usalama wa kutosha kusini, ambapo Israel imewataka kuhamia eneo ambalo imeteua kuwa eneo la kibinadamu.
Wengine wanasema hawana uwezo wa kuondoka, huku wengine wakitumai kuwa mkutano wa Jumatatu wa viongozi wa Kiarabu nchini Qatar utaishinikiza Israel kuachana na mpango wake wa kutaka kukalia kwa mababu maeneo yao.