Venezuela yazifunga balozi zake Norway, Australia
Venezuela imetangaza kufunga balozi zake nchini Norway na Australia, na kufungua mpya katika mataifa ya Burkina Faso na Zimbabwe, ikisema ni sehemu ya “mabadiliko ya kimkakati” ya huduma za kidiplomasia.