Mvutano unaongezeka kati ya White House na mamlaka ya Chicago. Rais wa Marekani Donald Trump kwa mara nyingine ametishia kuingilia kijeshi katika mji wa tatu kwa ukubwa nchini Marekani, unaotawaliwa na chama cha Democratic. Almechapisha ujumbe na picha yenye utata mkubwa akirejelea filamu ya Apocalypse Now, na kusababisha hasira ya viongozi wa majimbo ya Chicago na Illinois.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Picha inaonekana kuwa imetolewa na Akili Bandia. Inaonyesha rais, akiwa amevalia sare za kijeshi, dhidi ya mandhari ya moto na helikopta katika anga ya machungwa ya Chicago, na kichwa cha maneno: “Chipocalypse Now.” Rejeleo la wazi la filamu iitwayo Apocalypse Now kuhusu Vita vya Vietnam.

Juu kabisa ya picha, Donald Trump anapindisha mstari maarufu kutoka kwa filamu: “Ninapenda harufu ya kufukuzwa asubuhi na mapema.” “Chicago itaelewa kwa nini inaitwa Wizara ya Vita,” imeandikwa pia, ikirejelea jina jipya la Pentagon, Idara ya Ulinzi, lilitolewa na Donald Trump.

Chapisho hili, lililochapishwa kwenye Truth Social, jukwaa la rais wa Marekani, limemkasirisha gavana wa Illinois kutoka chama cah Democratic. “Huu si mzaha,” ameandika J.B. Pritzker kwenye mtandao wa kijamii wa X. “Rais wa Marekani anatishia kuingia vitani dhidi ya jiji la Marekani.” “Illinois haitatishwa na anayeweza kuwa dikteta,” ameongeza mwanademokrasia huyu mashuhuri.

Chicago, “mji mkuu wa mauaji duniani” kulingana na Donald Trump

Naye mbunge wa Chicago Mike Quigley amesema kushangazwa na maneno ya Donald Trump: “Hakika hiki ni kitendo cha jeuri, ni vitisho.” “Hii haina uhusiano wowote na kupambana na uhalifu katika jiji,” mbunge kutoka chama cha  Democratic ametangaza kwenye MSNBC.

Ni lazima isemwe kwamba hii si mara ya kwanza kwa Donald Trump kushambulia Chicago. Tayari ameita jiji hilo “shimo la panya” na “mji mkuu wa mauaji duniani.” Na kwa siku chache zilizopita, rais amekuwa akitishia kupeleka askari kutoka kikosi cha ulinzi wa taifa katika mji huo. Kikosi hiki cha kijeshi cha akiba tayari amekipeleka katika ngome zingine mbili za chama cha Democratic: Los Angeles na Washington, DC.

Wanajeshi waliovalia sare waliokuwa na magari ya kivita wamekuwa wakishika doria katika mji mkuu wa Marekani tangu katikati ya mwezi Agosti. Siku ya Jumamosi, Septemba 6, mamia, ikiwa si maelfu, ya watu waliandamana katika mitaa ya Washington kupinga “ukaaji” wa jiji hilo na askari wa shirikisho. “Huko Washington, uhalifu mkubwa uko katika Ikulu ya White House,” imeandikwa kwenye moja ya mabango.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *