
Hali ya wasiwasi bado inashuhudiwa Uvira, jimboni Kivu Kusini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambapo mwishoni mwa wiki iliyopita, kwa siku ya sita mfululizo mji huo ulisalia mahame.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Wapiganaji wa Wazalendo, wanataka serikali jijini Kinshasa, kumwondoa Jenerali Olivier Gasita, aliyetumwa katika eneo himo kwa madai kuwa, ana ushirikiano wa karibu na waasi wa AFC/M23 kwa kile anachoelezwa kuwa ni kutoka kwa jamii ya Banyamulenge.
Wazalendo wanaonekana katika maeneo mengi ya mji wa Uvira na maeneo ya jirani na kuapa kuhakikisha kuwa shughuli za kawaida, zinakwama, hadi pale Jenerali Gasita atakapoondolewa.
Hali inaendelea kuwa ya wasiwasi, huku wapiganaji wa Wazalendo wakiendelea kudhibiti maeneo mengi na kuzua hali ya sintofahamu kati yao na wanajeshi wa FARDC ni nani anayetakiwa kuaminiwa kuhusu usalama wa Uvira.
Wapiganaji wa Wazalendo na FARDC wamekuwa wakishirikiana katika vita dhidi ya waasi wa M23/AFC lakini katika ujio wa Jenerali Gasita, wametofautiana vikali.