
Katika Mkutano wa Pili wa kujadili Mabadiliko ya tabia nchi unaoendele nchini Ethiopia, Waziri Mkuu wa nchi hiyo Abiy Ahmed alitangaza kwa fahari ombi la Ethiopia kuwa mwenyeji wa COP 32 mnamo 2027, na kuualika ulimwengu kushuhudia uongozi wa Afrika katika suluhisho la hali ya hewa.
Mkutano wa Wanachama (COP) ndio chombo kikuu cha maamuzi cha Mkataba wa Mfumo wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (UNFCCC).
Waziri Mkuu Abiy aliwasilisha ‘Mpango wa Urithi wa Kijani wa Ethiopia’ kama mfano mkuu wa kujitolea kwa nchi hiyo katika kukabiliana na hali ya hewa.
“Mnamo mwaka wa 2019, tulizindua mpango wa ‘Green Legacy.’ Katika miaka saba, tumepanda zaidi ya miche bilioni 48. Inapoza ardhi yetu, inarutubisha udongo wetu, inarejesha vyanzo vya maji, hutoa chakula, kuunda nafasi za kazi, na kuongeza mauzo ya nje,” aliuambia mkutano huo unaofanyika Addis Ababa.
Waziri Mkuu alibainisha kuwa “upandaji miti si mradi wa majaribio, bali ni utamaduni,” akisisitiza kuwa hii ni juhudi endelevu, inayoendeshwa na jamii badala ya mpango wa muda.
Kila mwaka, wawakilishi kutoka nchi zote ambazo ni “Washiriki” katika Mkataba wa Paris hukusanyika ili kukagua maendeleo kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, kujadili makubaliano mapya, na kuweka malengo ya siku zijazo.
Nchi zilizowahi kuwa wenyeji wa COP Afrika
Kenya ilikuwa mwenyeji wa mkutano huu wa kimataifa mwaka 2006 jijini Naiorbi, Morocco ilikuwa mwenyeji 2001 na 2016.
Afrika Kusini ililkuwa mwenyeji 2011 na Misri 2022.