Waziri Mkuu wa Ufaransa François Bayrou amepoteza kura ya imani aliyoiitisha mwenyewe bungeni kufuatia mkwamo wa kisiasa kuhusu bajeti ya kubana matumizi.

Bayrou alipoteza kura hiyo Jumatatu usiku kwa kishindo baada ya wabunge 364 kumpinga dhidi ya 194 waliomuunga mkono, na kumwacha Emmanuel Macron akikabiliwa na shinikizo la kuteua waziri mkuu mpya wa saba katika kipindi cha urais wake ili kuzuia mgogoro wa kifedha na kisiasa, huku Ufaransa ikiingia katika hali ya sintofahamu.

Hali hiyo imeongeza wasiwasi wa wawekezaji baada ya gharama za mikopo ya Ufaransa kupanda juu ya zile za Italia, na wachambuzi wanasema Macron atalazimika kufanya maamuzi ya haraka kuepusha mkwamo wa kikatiba na kuyumbisha masoko.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *