Bunge nchini Ufaransa limepiga kura kuangusha serikali ya Waziri Mkuu François Bayrou, hatua inayokuja baada ya mkwamo uliodumu kwa miezi kadhaa kuhusu bajeti yake ya kubana matumizi.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Baada ya saa tatu za mjadala, wabunge wa Ufaransa siku ya Jumatatu wameiangusha serikali ya Waziri Mkuu François Bayrou, ambaye alikuwa akihudumu kwa kipindi cha chini ya miezi tisa. Bw. Bayrou atawasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa Rais wa Jamhuri ya Ufaransa, Emmanuel Macron, leo Jumanne asubuhi.

Ili kuiangusha serikali, kura nyingi zilizohitajika zilikuwa 280. Wabunge 364 katika Bunge la taifa walipiga kura ya kutokuwa na imani na François Bayrou, huku 194 pekee ndio waliomuunga mkono.

Wabunge walikuwa na dakika 30 za kupiga kura, na matokeo yalitangazwa karibu 12:50 saa za Ufaransa.

Emmanuel Macron aombwa kujiuzulu

Mara tu alipoondoka kwenye kikao kisicho cha kawaida cha bunge, kiongozi wa kundi la La France Insoumise (LFI), Mathilde Panot, alimlenga Rais Macron.

Hatukubaliani kabisa na sera yoyote ya Macroni, alitangaza, akibainisha kwamba chama chake kitawasilisha hoja ya kutokuwa na imani na rais wa Ufaransa mapema siku ya Jumanne.

Kiongozi mwenza wa chama cha siasa, Jean-Luc Mélenchon, almeeleza kufarijika kwa matokeo ya kura hiyo na kutangaza kuwa Macron sasa yuko mstari wa mbele kuwakabili wananchi. Yeye pia lazima aende, alisema kwenye ukurasa wake wa X.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *