Umoja wa Mataifa wafunga vituo vyake AfghanistanUmoja wa Mataifa wafunga vituo vyake Afghanistan
12 Septemba 2025

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwashughulikia wakimbizi UNHCR limefunga vituo vyake vinane Afghanistan, vinavyotoa huduma kwa wakimbizi waliorejeshwa nchini humo.

https://p.dw.com/p/50Poc

Afghanistan, Kabul
UN yafunga vituo vyake Afghanistan baada ya Taliban kuwanyima wanawake nafasi ya kuvifikiaPicha: Wakil Koshar/AFP

Hatua hiyo imechukuliwa kufuatia madai kuwa utawala wa Afghanistan kuwazuia wakimbizi wa kike kufikia vituo hivyo.

Umoja wa Mataifa umesema taifa jirani la Pakistan linawarejesha kwanguvu waafghan walioko  nchini humo nyumbani Afghanistan, ukionya kuwa takriban watu milioni moja huenda wakaathirika na hatua hiyo.

Wiki ya kwanza ya Septemba pekee wakimbizi 100,000 walirejeshwa Afghanistan.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *