Msemaji wa kamandi ya mashariki wa jeshi la China Kanali Shi Yi amesema vikosi vya anga na vya wanamaji vya China vilifuatilia mwenendo wa meli mbili za Marekani na Uingereza na kudai zilidhoofisha amani na utulivu eneo hilo.

Marekani na Uingereza zinautazama Mlango Bahari wa Taiwan kama eneo la maji ya kimataifa linaloweza kutumiwa na meli kutoka mataifa yote. Hata hivyo China inadai Taiwan ni sehemu ya himaya yake na inadai mamlaka katika eneo la maji linalotenganisha Kisiwa hicho kinachojitawala na China bara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *