Ameutangaza uamuzi huo saa chache baada ya kumteua na kumuapisha Waziri Mkuu mpya wa mpito aliyewahi kuwa Jaji Mkuu nchini humo, Sushila Karki. Karki mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo Nepal, ameteuliwa baada ya majadiliano ya kina kati ya Rais Poudel, Mkuu wa jeshi Ashok Raj Sigde, na viongozi wa maandamano makubwa yaliyosababisha vifo vya takriban watu 51. 

Maandamano hayo yalichochewa na uamuzi wa serikali ya Nepal wa kuipiga marufuku mitandao kadhaa ya kijamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *