Rubio anatarajiwa kujadili kwa undani vita hivyo na viongozi wa Israel pamoja na athari zake katika juhudi za usitishaji vita Gaza.

Rubio aliyasema hayo licha ya Israel kuishambulia Qatar kwa madai ya kuwalenga viongozi wa Hamas, shambulio lililokosolewa vikali kote duniani.

Kabla ya kuondoka Marekani Rubio alisema japokuwa Trump hajafurahishwa na kitendo cha Israel kushambilia Qatar, tukio hilo halitobadilisha uhusiano uliopo kati ya mataifa hayo mawili.

“Uhusiano wa Marekani na Israel ni imara. Unaendelea kuwa imara. Rais anataka mzozo huu umalizike na anataka mateka warejeshwe nyumbani. Wote 48 waliokufa na walioko hai. Ni wazi kwamba tuna wasiwasi na matukio ya wiki iliyopita, rais hakupenda kilichotokea. tutalizungumzia hilo na athari zake katika kuwaokoa mateka wote, kulisambaratisha kundi la Hamas pamoja na kusitisha vita. Hicho ni kipaumbele cha rais,” alisema Rubio.

Hili ni shambulio la kwanza kufanywa na Israel kwa washirika wake na limeweka doa katika juhudi zinazoendelea za kutafuta suluhu ya kudumu katika mgogoro wa Gaza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *