
Shirika hilo limesema zaidi ya waaghan milioni 2 wamerejeshwa nyumbani kutoka nchi jirani tangu mwanzoni mwa mwaka huu.
IOM imesema wengi walirejeshwa kinyume na matakwa yao na wengi wao pia hawajawahi kuishi Aghanistan tangu walipoitoroka nchi iliyoko chini ya uongozi wa kundi la Taliban lililo na itikadi kali.
Mihyung Park, Mkuu wa IOM anayeratibu mipango ya Afghanistan amesema wanawake walioko nchini humo bado wananyimwa nafasi ya kuendelea na masomo na kunyimwa nafasi kubwa za ajira.
Amesema wanawake waliokuwa wakishikilia nafasi za juu serikalini, waandishi habari au wanaharakati wa kutetea haki za binaadamu wote wapo hatarini hasa baada ya Taliban kurejea madarakani.