
Waziri Mkuu huyo mpya wa kwanza wa kike nchini humo, ametangaza kuwa kila familia iliyopoteza wapendwa wao kutokana na maandamano hayo, itapokea fidia ya dola 11,330 na kusistiza kuwa waliojeruhiwa pia watashughulikuwa.
Maandamano makubwa yaliyoitishwa na vijana wa Gen Z yalianza Septemba 8 baada ya serikali kufungia mitandao kadhaa ya kijamii.
Baadae maelfu ya vijana hao waliojaa hasira waliteremka barabarani kupinga pia ufisadi na umasikini.
Maandamano yaligeuka na kuwa ya virugu hali iliyomlazimisha waziri mkuu aliyekuwepo Khadga Prasad Oli, kujiuzulu na kuitoroka nchi.