Uchaguzi huo unaangaliwa kama kipimo kwa serikali ya muungano ya Kansela Friedrich Merz, unaojumuisha muungano wa kihafidhina wa vyama vya Christian Democratic Union, CDU na Christian Social Union CSU na Chama cha siasa za wastani zinazoegemea mrengo wa kushoto cha SPD.

Uchaguzi huu ni wa kwanza tangu Merz alipoingia madarakani mwezi Mei. Kansela huyo amesema anafuatilia matokeo ya uchaguzi huu kwa makini kujua kile wapiga kura wanachokitaka katika siasa za kikanda na kitaifa.

Waangalizi wa uchaguzi huu pia watakuwa wanakifuatilia Chama kinachofuata siasa kali za mrengo wa kulia nchini Ujerumani, AfD, ambacho kimekuwa kikipata ushindi katika chaguzi za hivi karibuni na kuwa chama cha pili kikubwa cha kisiasa katika ngazi ya taifa mwaka huu.

Licha ya wafuasi wake wengi kutokea Mashariki mwa Ujerumani, AfD inamatumaini ya kutanua umaarufu wake upande wa Magharibi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *