Serikali inayoungwa mkono na jeshi la Sudan, imetupilia mbali pendekezo jipya la amani lililotolewa na mataifa manne ya magharibi yenye ushawishi, ikisema mzozo wa nchi hiyo utatatuliwa na raia wa nchi hiyo.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Ijumaa, Marekani, Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu na Misri kwa pamoja zilitoa wito wa kusitishwa kwa mapigano, kuruhusiwa kwa misaada ya kibinadamu na kurejeshwa kwa utawala wa kiraia.

Aidha mataifa hayo katika mapendekezo yao, walikataa jukumu lolote la jeshi katika serikali ya mpito ya Sudan itakayoundwa baada ya vita kumalizika.

Katika majibu yake, serikali ya Sudan ilisema inakaribisha juhudi za kumaliza vita, lakini haitakubali “uingiliaji kati ambao hauheshimu mamlaka ya taifa hilo na taasisi zake halali, ambazo zinaungwa mkono na watu wa Sudan.

Mwezi Mei, jeshi liliunda serikali mpya ya mpito ya kiraia, hatua iliyojibiwa na RSF kwa  kuunda serikali mbadala, hali iliyochochea mgogoro zaidi.

Licha ya juhudi za mara kwa mara za kimataifa za kusuluhisha mzozo wa nchi hiyo, pande zote mbili zimeonyesha nia kidogo ya kufikia suluhu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *