Kampeni za uchaguzi mkuu wa rais nchini Malawi, zilitamatika mwishoni juma tayari kwa zoezi la siku ya Jumanne ambapo raia wa nchi hiyo watachagua kati ya marais wawili wanaowania kuchaguliwa kwa muhula wa pili.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi wa Jumanne wa rais na wabunge unakuja huku nchi hiyo ya kusini mwa Afrika ikiwa katika mzozo wa kiuchumi, unaochochewa na uhaba wa mafuta, fedha za kigeni, athari za ukame na vimbunga.

Akihitimisha kampeni zake mjini Lilongwe, rais wa sasa Lazarus Chakwera, aliwaambia raia na wafuasi wa chama chake cha Congress, kuwa amesikia kilio chao na kwamba akichaguliwa atarekebisha mambo.

Kwa upande wake mgombea anayepewa nafasi ya kumshinda Chakwera, rais wa zamani Peter Mutharika, yeye alitumia madhila wanayopitia raia wa nchi hiyo kuwashawishi wamchague kwa mara nyingine baada ya kushindwa katika uchaguzi wa marudio wa mwaka 2020.

Katika uchaguzi uliopita, Chakwera alishinda kwa asilimia 59 tu ya kura zote, wadadisi wa mambo wakisema tuhuma za rushwa, upendeleo na hali mbaya ya uchumi iliyoshuhudiwa tangu aingie madarakani, huenda vikamuangusha.

Wagombea wengine 17 wanatarajiwa kushiriki uchaguzi wa Jumanne.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *