Rais wa zamani wa Malawi Peter Mutharika anaendelea kuongoza dhidi ya mpinzani wake, rais aliyeko madarakani Lazarus Chakwera katika uchaguzi mkuu wa rais wa taifa hilo la kusini mwa Afrika, kulingana na matokeo ya awali kutoka theruthi mbili ya mabaraza.

Mutharika anaongoza kwa asilimia 66 ya kura halali kwenye mabaraza 24 kati ya 36 katika uchaguzi wa Septemba 16, ikilinganishwa na asilimia 24 alizopata Chakwera. Mgombea anahitaji kupata zaidi ya asilimia 51 ya kura ili kutangazwa mshindi wa moja kwa moja, vingenevyo kutakuwa na duru ya pili ya uchaguzi.

Wachambuzi wa kisiasa walikuwa wametabiri kwamba Mutharika aliye na umri wa miaka 85 ambaye amewahi kuiongoza Malawi kati ya mwaka 2014-2020, angetoa upinzani mkali kwa Chakerwa anatafuta kuchaguliwa tena.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *