
Akizungumza Jumanne katika Umoja wa Mataifa, Macron amesema katika eneo la Maziwa Makuu, mamlaka na uadilifu wa eneo la Kongo lazima uheshimiwe.
Kulingana na Macron, wanapaswa kurejesha matumaini ya wakaazi wa Kivu na kwa maelfu ya watu ambao wamelazimika kuyakimbia makaazi yao.
Mkutano huo utakaofanyika Paris, utawaleta pamoja wote ambao wanaweza kushughulikia dharura ya kiutu na kuchangia katika juhudi na mipango ya amani ambayo tayari inaendelea.
Baada ya mazungumzo ya miezi mitatu nchini Qatar, waasi wa M23 na serikali ya Kongo waliazimia kusitisha mapigano baada ya kusaini makubaliano Julai 19, kufuatia makubaliano mengine ya amani yaliyosainiwa mjini Washington kati ya serikali ya Kongo na Rwanda mwishoni mwa mwezi Juni.