
Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti kuwa watu 400 wameaga dunia kw autapiamlo katika Ukanda wa Gaza kutokana na njaa ya makusudi iliyosaabishwa na Israel. Watoto 100 ni miongoni mwa idadi hii tajwa ya waliopoteza maisha kwa njaa; watoto 80 walikuwa na umri wa chini ya miaka mitano.
Dakta Rana Abu Zaatir Mkuu wa Idara ya Tiba Lishe katika Hospitali ya Al-Awda kaskazini mwa Gaza amesema: Wagonjwa wengi wanafika hospitalini kutoka kusini mwa Ukanda wa Gaza na katika maeneo ya kusini mwa ukanda huo.
Pamoja na kuongezeka idadi ya watu wenye utapiamlo wakiwemo pia watoto walio na umri chini ya miaka mitano lakini hospitali ya Al-Awda imeanza kupokea wagonjwa na kesi mpya za watoto wenye utapiamlo waliopindukia umri wa miaka mitano.
Hivi sasa, kuna vituo vinne vya kushughulikia tatizo la utapiamlo huko Gaza ambavyo vinaendelea kufanya kazi. Hii ni katika hali ambayo maeneo ya kaskazini mwa Gaza pia yamekatiwa misaada ya chakula kwa muda wa wiki moja sasa na hivyo kutatiza huduma za matibabu lishe kwa waliokumbwa na utapiamlo.
Dakta Zaatir anasema kuna idadi kubwa ya watoto na watu wazima walioaga dunia kwa utapiamlo na matatizo mengine ya kiafya yanayosababishwa na ukosefu wa chakula.
“Kwa bahati mbaya, katika siku zijazo na hata katika kipindi kijacho, ikiwa vivuko vitaendelea kufungwa na bei za bidhaa muhimu za mahitajio kuendelea kupanda tutakabiliwa na maafa halisi katika Ukanda wa Gaza kutokana na utapiamlo na ukosefu wa chakula cha kutosha cha kuweka kuishi maisha ya kawaida ya watu wa Gaza.
Leo Jumatatu, Mpango wa Chakua Duniani (WFP) umeeleza ufikishaji misaada Ukanda wa Gaza umekuwa ukiimarika hata hivyo mchakato wa kufikisha misaada ya kibinadamu upande wa kaskazini unapasa kurejeshwa haraka iwezekanavyo.