Wanajeshi vya Yemen wamefanya shambulio la ndege isiyo na rubani (droni) kuelekea mji wa bandari wa Eilat katika ncha ya kusini kabisa ya maeneo yanayokaliwa na Israel katika operesheni mpya ya jeshi la Yemen ya kulipiza kisasi katika kuwaunga mkono wananchi wa Palestina wa Ukanda wa Gaza.

Jeshi la Israel limedai katika taarifa yake kuwa upo uwezekano droni ya jeshi la Yemen ilitunguliwa wakati ilipokuwa ikiruka katika anga ya Bahari Nyekundu. 

Shambulio hili tajwa la droni kutoka Yemen ni la pili kufanywa na vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo katika muda wa siku moja. Msemaji wa jeshi la Yemen amesema kuwa oparesheni hiyo ya jeshi la Yemen inaweza kufikia malengo yake yaliyokusudiwa. 

Vikosi vya ulinzi vya Yemen vinatekeleza vizuizi vya kimkakati vya baharini kwa lengo la kuzuia silaha na zana za kijeshi kutumwa kwa utawala haramu wa Israel huku vikitoa mwito kwa jamii ya kimataifa kukabiliana na maafa makubwa ya kibinadamu huko Gaza.  

Wakati huo ho, jeshi la Yemen limefanya mashambulizi kadhaa ya makombora na droni katika maeneo nyeti ya Israel katika kuonyesha mshikamano wao na Wapalestina wa Ukanda wa Gaza. 

Jeshi la Yemen limetangaza azma yake ya kuendeleza oparesheni hadi hapo Israel itakapositisha mashambulizi ya anga na nchi kavu dhidi ya Gaza. 

Wizara ya Afya ya Gaza imetangaza kuwa, Wapalestina 67,139 wameuliwa shahidi  wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto wadogo tangu Israel ianzishe vita na mauaji ya kimbari dhidi ya Gaza Oktoba 7 2023.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *