#HABARI: Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba, amekutana na wataalam kutoka Tume ya Taifa ya Mipango wakiongozwa na Naibu Katibu Mtendaji – Menejimenti ya Utendaji na Tathmini, Dkt. Linda Ezekiel kwa lengo la kujadili namna ambavyo Wizara na Taasisi zake zimejipanga kutekeleza miradi ya kimkakati ya nishati inayochangia katika kufanikisha malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Msingi wa kikao hicho umetokana na Sekta ya Nishati kuainishwa katika Dira 2050 kuwa ni moja ya vichocheo vitano vitakavyoongeza kasi ya kufikia malengo ya Dira hiyo, ikielezwa kuwa Nishati ya uhakika ni nyenzo muhimu katika kuchochea maendeleo ya viwanda na shughuli mbalimbali za kiuchumi ili kuboresha viwango vya maisha kwa kutoa fursa za ajira kwa maendeleo endelevu katika jamii.

Katika kikao hicho kilichofanyika jijini Dodoma na kuhusisha Watendaji kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati,
Mha. Mramba amesema pande hizo mbili zimejipanga kuimarisha uratibu wa utekelezaji wa miradi ya nishati ili kuhakikisha kuwa inalingana na vipaumbele vya kitaifa vya maendeleo.

“Wizara ya Nishati inaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya nishati ukiwemo mradi wa kusafirisha umeme wa kV 400 wa Chalinze–Dodoma, ambao unatarajiwa kukamilika Juni 2026. Huu ni moja ya miradi itakayoleta chachu ya kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika katika mikoa ya Katavi, Kigoma na maeneo mengine ambayo yamekuwa yakikabiliwa na changamoto za upatikanaji wa umeme thabiti.” Amesema Mhandisi Mramba

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KISHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *