#HABARI: Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Madini kufanya ufuatiliaji wa makampuni ya madini ambayo yameshikilia maeneo kwa muda mrefu lakini hawajayaendeleza mpaka sasa yakiwemo makampuni matatu wilayani Ruangwa.

Ametoa agizo hilo alipotembelea kampuni ya uchimbaji wa madini Huaer International Limited katika Kijiji cha Ng’au Ruangwa mkoani Lindi ambapo amesema kuwa makampuni ya Nachu, Uranex na Paco Gems Ltd yanapaswa kusema hatma ya maeneo waliyoyahodhi kwa muda mrefu vinginevyo ardhi hiyo itarudishwa kwa wananchi.

Mheshimiwa Majaliwa ameipongeza kampuni ya Huaer International Limited ambayo imefanikiwa kuanza mchakato wa uwekezaji ndani ya kipindi kifupi baada ya kupata vibali vyote muhimu.

#KambiYaMichezo

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *