Miradi mikubwa ya maendeleo iliyoanzishwa katika awamu ya tano imekamilika kwa kiasi kikubwa, amesema Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na wananchi wa Misungwi mkoani Mwanza leo Jumanne, Oktoba 7, 2025.
Dkt. Samia amesema miradi hiyo ni pamoja na daraja la Kigongo–Busisi, Reli ya Kisasa – SGR, na meli ya MV Mwanza ambayo sasa ipo katika majaribio kwenye Ziwa Victoria.
Aidha, amewashukuru wakazi wa Misungwi kwa kujitokeza kwa wingi, akisema mwitikio huo unaonyesha imani yao kwa CCM na viongozi wake.
✍ @claud_jm
#AzamTVUpdates