Shambulio hilo limetokea katika eneo la magharibi mwa nchi hiyo, tukio ambalo linahusishwa na wanamgambo wa Kikurdi.

Shambulio hilo lilitokea Jumatatu usiku na kulenga jengo linalomilikiwa na kundi la wapiganaji wanaoiunga mkono serikali, karibu na mji wa Sarvabad katika mkoa wa Kurdistan.

Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la IRNA, wanachama wengine watatu wa IRGC walijeruhiwa katika shambulio hilo.

Ingawa wahusika wa shambulio hilo bado hawajatambuliwa rasmi, mamlaka za Iran zimewalaumu wale waliwaita “kundi linalopinga mapinduzi.”

Iran mara nyingi hutumia istilahi hiyo kumaanisha makundi ya waasi wa Kikurdi wanaoendesha operesheni zao kando ya mpaka na Iraq.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *