Lecornu anasema kuna nia ya pamoja ya kupitisha bajeti kufikia mwishoni mwa mwaka. Waziri Mkuu huyo anasema atakutana na Rais Emmanuel Macron baadae Jumatano kujadiliana kuhusu matokeo ya mazungumzo yake na vyama hivyo vya kisiasa.

Awali waziri mkuu wa zamani na mwandani wake wakati mmoja Edouard Philippe alikuwa amemtaka Rais Macron ajiuzulu.

Philippe amesema uchaguzi nchini humo unastahilikuandaliwa mara tu bajeti itakapopitishwa.

Uchaguzi ufuatao nchini Ufaransa ambao mwanasiasa wa siasa kali za mrengo wa kulia Marin Le Pen anaona ana nafasi nzuri zaidi ya kuchukua mamlaka unatarajiwa kufanyika mwaka 2027, huku Macron akiwa hawezi kugombea tena urais, na Philippe akiwa tayari ashatangazwa kuwa mgombea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *