Waziri Mkuu wa Qatar na mwenzake wa Uturuki, wanajiunga na wajumbe kutoka Hamas na Israeli katika mji wa pwani wa Sharm El-Sheikh, nchini Misri kushiriki kwenye mazungumzo kuhusu mkataba uliopendekezwa na Marekani, kumaliza vita kwenye ukanda wa Gaza.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo haya yanaendelea kwa siku ya tatu mfululizo, ambapo wajumbe wanashauriana kuhusu hoja zote 20 zilizopendekezwa na rais Donald Trump, ili kumaliza vita vinavyoendelea kwa mwaka wa pili kwenye ukanda wa Gaza.

Wakati wajumbe zaidi wakiongezeka, kutoka Qatar na Uturuki, rais Trump amesema, wajumbe wa Marekani nayo pia wapo kwenye mazungumzo hayo na kuonesha matumaini makubwa ya mwafaka kupatikana.

Miongoni mwa mapendekezo yanayojadiliwa ni kuachiwa huru kwa mateka wote, walio hai na waliokufa lakini pia usitishwaji vita kwenye ukanda wa Gaza ambavyo vimesababisha mauji ya Wapalestina zaidi ya elfu 67.

Mazungumzo haya yanaendelea wakati huu ikiwa imepita miaka miwili baada ya Israel kushambuliwa na Hamas, na baadaye kuzuka kwa vita vinavyoendelea mpaka leo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *