
Hatimaye RFI imebaini kuwa awamu ya sita ya mazungumzo kati ya serikali ya DRC na waasi wa AFC/M23, itafanyika kuanzia wiki ijayo nchini Qatar.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mazungumzo hayo yaliyotarajiwa kuanza wiki hii, yameahirishwa hadi wiki ijayo kutoka na ombi la wapatanishi kutoka Qatar.
Lengo ya mazungumzo hayo, ni kuendelea kujadiliana namna ya kupata makataba wa kudumu, ili kusitisha vita vinavyoendelea jimboni Kivu Kusini na Kaskazini.
Ripoti zinasema, kushirikishwa kwa jeshi la kulinda amani MONUSCO kusaidia kupata suluhu, linasalia suala tata kwenye mazungumzo hayo.
Waasi wa AFC/M23, hawana imani na MONUSCO.
Wanadiplomasia kutoka nchi za Magharibi wanasema pande zote zinapaswa kuonesha utayari wa kutekeleza mapendekezo kutoka kwa wasuluhishi ili kupata mkataba wa kudumu, utakaoleta amani.
Mara ya mwisho lwa mazungumzo haya kufanyika ilikuwa mwezi Agosti, ambapo wajumbe wa serikali na waaasi wa AFC/M23 walijadiliana namna ya kubadilishana wafungwa.