
Rais wa Marekani Donald Trump amesema pande hasimu kwenye mzozo wa Gaza zimekubaliana kuhusiana na awamu ya kwanza ya mpendekezo yake ya upatikanaji wa amani huko Gaza.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Baada ya kuthibitisha kuwa Hamas na Israel zimekubaliana kuhusu awamu ya kwanza ya mapendekezo kuelekea upatikanaji wa amani huko Gaza, Rais wa Marekani Donald Trump amesema mateka wote wa Israel wanaozuiliwa huko Gaza wataanza kuachiwa hivi karibuni.
Naye Benjamin Netanyahu– Waziri Mkuu wa Israel amesema watawarejesha nyumbani mateka wote wanaoshikiliwa na Hamas katika Ukanda wa Gaza.
Tangazo lake limejiri baada ya Rais wa Marekani Donald Trump, mshirika mkubwa wa Israel kutangaza kuwa makubaliano yamefikiwa kumaliza vita vya Gaza.
Hatua hiyo ya kuafikiwa kwa makubaliano pia imethibitishwa na wapatanishi kwenye mzozo huo.