Makamanda wa jeshi la Pakistan wamebainisha matarajio yao kuhusu kusitishwa vita haraka iwezekanavyo huko Gaza na kutumwa misaada ya kibinadamu katika eneo hilo na kusisisitiza kuwaa Pakistan inaendelea kuunga mkono bila masharti suala la kuasisi nchi huru ya Palestina.

Mkutano wa 272 wa Pamoja wa Makamanda wa Jeshi umefanyika leo ukiongozwa na Asim Munir, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Pakistan.

Makamanda wa jeshi la Pakistan wamechunguza matukio ya usalama wa ndani na viitisho kutoka nje na kusisitiza kuimarisha uwezo wa kukabiliana na uvamizi na kujiimarisha kijeshi na kiufundi katika mapambano dhidi ya ugaidi. 

Makamanda wa jeshi la Pakistan wamekumbusha matamshi ya karibuni ya wakuu wa kijeshi na kiulinzi wa India na kutahadharisha kuwa chokochoko zozote za nchi ajinabi zitakabiliwa na jibu la haraka, makini na kali la Pakistan. 

Makamanda wa Pakistan wanaamini kuwa, hatua za kupenda vita na kujitanua zisizo na msingi zitashadidisha mivutano na kuuweka hatarini usalama na amani wa kanda hii. 

Wakuu wa jeshi la Pakistan wamesisitiza kuhusu umuhimu wa mazungumzo ya karibuni ya kidiplomasia ya nchi hiyo na kusisitiza juu ya njia njema ya Islamabad katika uga wa kikanda na kimataifa.  

Maafisa wa kijeshi wa Pakistani walikubali umuhimu wa mazungumzo ya hivi karibuni ya ngazi ya juu ya kidiplomasia ya nchi hiyo na kusisitiza jukumu la Pakistan mkabala wa amani ya kikanda na kimataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *