Mgombea wa urais kupitia CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema serikali ya awamu ya sita imeongeza pato la wavuvi kutoka shilingi bilioni 9.4 hadi bilioni 38.4 katika kipindi cha miaka mitano, hatua iliyoongeza ajira na kipato cha wananchi.

Akizungumza Bunda Mjini, mkoani Mara, Dkt. Samia ameahidi kuendeleza sekta za uvuvi, kilimo na viwanda vya kuchakata mazao, sambamba na ujenzi wa skimu za umwagiliaji na mabwawa ili kuongeza uzalishaji.

Amesema Bunda imechangia utoshelevu wa chakula nchini kwa kufikia asilimia 128.

✍️ @claud_jm

#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *