Baada ya Israel na Hamas kufanya mkutano nchini Misri kujadili suluhisho la kudumu la amani katika Ukanda wa Gaza, pande hizo mbili zimekubaliana kuanza kutekeleza baadhi ya vipengele 20 vilivyopendekezwa katika mpango wa amani wa Trump.
Miongoni mwa vipengele hivyo, wameafikiana kuanza na awamu ya kwanza inayohusisha kuwarejesha mateka kutoka pande zote mbili kama ishara ya kujenga imani na kuanzisha mazingira ya mazungumzo ya kina zaidi.
Mchambuzi wa siasa za kimataifa, Ibrahim Rahbi, anafafanua kwa kina kuhusu makubaliano hayo na hatua zinazotarajiwa kufuata.
#AzamTVUpdates
✍Juliana James
Mhariri | John Mbalamwezi