Sayyid Abdul Malik Badreddin al-Houthi, kiongozi wa Ansarullah ya Yemen amesisitiza kuwa, utawala wa Kizayuni umefanya jinai za karne huuko Gaza kwa kutumia silaha za Marekani.

Sayyed Abdul Malik Badreddin al-Houthi amesema hayo katika hotuba yake kwa mnasaba wa mwaka wa pili wa Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa na mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wasio na hatia wa Gaza. Kiongozi huyo wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen ameyataja mashambulizi hayo kuwa ni jinai ya karne na kusisitiza uungaji mkono kamili kwa wananchi wa Palestina.

Aidhha katika hotuba yake hiyo ameashiria hali mbaya ya vita vya Gaza na kuongeza kuwa, utawala wa Israel na serikali ya Marekani umeua na kujeruhi asilimia 11 ya wakazi wa Gaza kutokana na mashambulizi yao ya kinyama, takwimu ambazo hazijawahi kushuhudiwa katika zama hizi.

Amelaani vikali mashambulizi yaliyolenga waandishi wa habari, wafanyakazi wa misaada, na vikosi vya ulinzi wa raia huko Gaza na kusisitiza: “Adui Mzayuni ameyalenga makundi yote ya watu wa Gaza kwa ukatili na uhalifu usio na kifani.”

Al-Houthi pia ameashiria matukio ya jinai za utawala wa Kizayuni zikiwemo za kutumia mbwa dhidi ya vikongwe na wagonjwa, kuteswa wafungwa na mateka  na kuuawa shahidi wengi wao kutokana na mateso hayo na kuongeza: “Uhalifu, uchokozi na ukiukwaji wa haki za binadamu uliofanywa na adui Israel unahesabiwa kuwa ni jinai kwa mujibu wa viwango vya sheria na makubaliano ya kimataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *