Mbunge wa jimbo la Nkulumane nchini Zimbabwe, Desire Moyo amefariki dunia mapema leo Ijumaa baada ya gari alilokuwa amepanda na wabunge wengine wanne kumgonga tembo karibu na eneo la Shangani kwenye barabara kuu ya Jiji la Harare na Bulawayo.

Wabunge hao walikuwa wakirejea kutoka Bungeni jijini Harare.

Mbunge huyo aliyekuwa akiutumikia wadhifa huo kwa muhula wa kwanza alithibitishwa kufariki dunia papo hapo huku wenzake wakijeruhiwa.

Kabla ya kuwa mbunge, Moyo alikuwa mwalimu na mshairi aliyefahamika na kuwa na sifa nchini humo akifahamika kwa jina la usanii la Moyoxide.

Wabunge walionusurika katika ajali hiyo in Madalaboy Ndebele, Rittah Ndlovu, Sethulo Ndebele na Libion Sibanda ambao walitibiwa wajeraha yao katika hospitali kuu ya Gweru.

Imetafsiriwa na @moseskwindi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *