Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Oktoba 10, 2025, amezuru kaburi la Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, na kuweka shada la maua.

Dkt. Samia alizuru kaburi hilo lililopo katika kijiji cha Mwitongo, Butiama, Mkoani Mara, akiwa ameambatana na viongozi wengine wa CCM, wakiwemo Katibu Mkuu, Balozi Asharose Migiro na Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara, Stephen Wasira.

Dkt. Samia pia amezungumza na familia ya Hayati Mwalimu Nyerere, akisisitiza umuhimu wa kuendeleza urithi na maadili ya Baba wa Taifa.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *