Mwendesha mashtaka wa serikali Ann Fransen, amewaambia waandishi wa habari kwamba vijana hao walikamatwa katika mji wa kaskazini wa Antwerp kama sehemu ya uchunguzi wa jaribio la mauaji ya kigaidi na kushiriki katika shughuli za kundi la kigaidi.

Ofisi ya mwendesha mashtaka haikufichua shabaha ya shambulizi

Hata  hivyo ofisi hiyo ya mwendesha mashtaka ilikataa kutaja shabaha zilizokusudiwa, lakini vyanzo vya karibu na waziri mkuu vimelithibitishia shirika la habari la AFP kwamba De Wever alikuwa miongoni mwao.

Waziri wa Mambo ya Nje Maxime Prevot amelitaja tukio hilo kuwa la kushtua na akazishukuru huduma za usalama na idara ya mahakama kwa kuchukuwa ambazo anasema zimesaidia kuzuia hali mbaya zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *