Nyumba zenye kufuga kasuku, mara nyingi zinahusishwa na utajiri na maisha ya kifahari. Na Afrika imebahatika kuwa mwenyeji wa aina ya kasuku ambaye ni maarufu zaidi.

Katika zaidi ya aina 10 ya ndege hawa barani Afrika, kasuku wa Kiafrika wenye rangi ya kijivu anajulikana zaidi hasa kwa kuwa  ni kati ya ndege wenye akili zaidi duniani. Kwa sasa anajulikana kama kasuku wa kijivu au kasuku wa kijivu wa Congo.

Ana rangi ya kijivu na nyeusi, na manyoya mekundu mkiani. Ana uzito wa gramu 400 na anaweza kuwa na urefu hadi kufikia sentimita 33.

Jinsia zote mbili zina muonekano sawa. Utafiti wa kasuku wa Kiafrika wa kijivu umeonyesha kuwa aliyekomaa ana kiwango cha akili sawa na mtoto mchanga.

Utafiti pia umegundua kuwa kasuku hawa wanaweza kutambua, kuomba, kukataa, kuainisha, na kuhesabu zaidi ya vitu 80 tofauti, na kujibu maswali kuhusu dhana ya rangi na umbo.

Kasuku wa kijivu wanapatikana hasa Afrika Magharibi na Kati ikiwa ni pamoja na Angola, Cameroon, Congo, Gabon, Ivory Coast na Ghana.

Katika Afrika Mashariki wanapatikana Kenya, Uganda na Kaskazini-magharibi mwa Tanzania.

Katika makazi yao ya asili, kasuku wa Kiafrika wa kijivu wanaweza kusafiri hadi kilomita 10 kwa siku.

Ndege hawa kawaida wanakuwa na jike mmoja tu, ikiwa na maana kwamba, wao huwa katika mahusiano na jike mmoja kwa wakati mmoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *