Wakazi wa jiji la Toyoake, lililoko katikati ya Japan, wameanza kutoa maoni yao kuhusu mwongozo mpya unaopendekeza kupunguza matumizi ya simu za mkononi kwa saa mbili kwa siku, ili kulinda afya ya akili na mahusiano ya kijamii.
Sheria ndogo ya jiji hilo, ambayo haina adhabu kwa atakayezidisha muda uliopendekezwa, haizingatii muda unaotumika kwa kazi au masomo, na inalenga kukuza tabia njema katika matumizi ya kidijitali miongoni mwa wananchi.
“Hata kwenye treni, kila mtu anatabasamu kwenye simu zao, na hakuna wanaozungumza…sihisi kama hili linapaswa kuwa jambo la kawaida,” – Amesema Meya wa jiji hilo, Masafumi Kouki.
Amesema mwongozo huu ni fursa kwa wakazi kutafakari jinsi wanavyotumia simu zao, na kujua kama wanazidi muda unaopendekezwa.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi