Wadau wa elimu nchini wamehimizwa kuungana katika kuwezesha upatikanaji wa miundombinu mbalimbali ya elimu ikiwemo viti vya waalimu, madawati pamoja na mabweni ya wanafunzi hali itakayosaidia kurahisisha ufundishaji na ujifunzaji na hivyo kuboresha ufaulu katika shule ya sekondari Isalalo ya Mbozi mkoani Songwe.
Wito huo umetolewa wakati wa mahafali ya kidato cha nne na mwanahabari Alumanus Mwasenga na kusisitizwa na makamu mkuu wa shule hiyo Amelye Ngunyule.
Mhariri @moseskwindi