Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kujenga nguvu kazi yenye ujuzi wa kisasa ili kushindana katika soko la ajira la kikanda na kimataifa.
Akifungua Kongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Julius Nyerere, kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan, amesema msingi wa maendeleo ni watu wenye elimu, ubunifu na maadili.
Amezitaka taasisi za elimu, sekta binafsi na viwanda kushirikiana kukuza stadi za kazi kufikia malengo ya Dira ya Taifa 2050.
✍ @claud_jm
#AzamTVUpdates