#HABARI: Mgombea Mwenza wa Rais Samia Suluhu Hassan katika kinyang’anyiro cha Urais wa Tanzania katika mwaka huu kupitia Chama cha Mapinduzi Dkt.Balozi Emmanuel Nchimbi leo ananya ziara ya siku mbili ya Kampeni mkoani Kigoma kuanzia Oktoba 12 na 13.

Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa CCM Mkoa wa Kigoma, Deogratius Nsokolo amesema Dkt. Nchimbi atapokelewa na wana-CCM na wananchi katika Uwanja wa Ndege wa Kigoma leo ktoba 12 ambapo baada ya kusalimiana na wananchi wa Kigoma mjini ataelekea Wilaya ya Kakonko ambako atakuwa na mkutano wa hadhara.

Katika mkutano huo wa kampeni ambao utafanyika mjini Kakonko Mgombea mwenza wa CCM atautumia kuomba kura kwa wagombea wa CCM, Mgombea Urais wa CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mgombea Ubunge katika jimbo la Kakonko Allan Mvano na wagombea udiwani kupitia ccm kutokakata 13.

Uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na Madiwani utafanyika Oktoba 29 mwaka huu ambapo mkoa wa Kigoma una majimbo nane ya uchaguzi na Kata 139.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *