Mgombea Ubunge wa Arusha Mjini kupitia CCM, Paul Makonda, amewataka waendesha bodaboda na bajaji nchini kutumia nafasi yao ya kusafirisha abiria kuhamasisha kura kwa wagombea wa CCM, akiwemo mgombea urais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza leo Oktoba 12, 2025 katika eneo la Mbogwe, mkoani Geita, Makonda amesema kundi hilo lina nafasi kubwa ya kuwa mabalozi wa maendeleo kwa kuelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kuchagua viongozi wa chama hicho.

✍ Mwandishi Wetu
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *