
Rais wa Madagascar Andry Rajoelina amehutubia taifa jioni ya Jumatatu, Oktoba 13, katika matangazo ya video kwenye mitandao ya kijamii. Mkuu wa nchi, anayepingwa sana na wakazi wake na sehemu ya jeshi, anabaini kwamba kuna “njia moja tu ya kutatua” mgogoro huu mkubwa nchini Madagascar, yaani “kuheshimu Katiba.” Andry Rajoelina hajatoa taarifa zozote kuhusiana na aliko.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Andry Rajoelina hatimaye amezungumza moja kwa moja jioni ya Jumatatu, Oktoba 13, baada ya kuchelewa saa tatu klingana na ratiba iliyopangwa. Ametoa ujumbe wake kwa wananchi wake, haswa kupitia ukurasa wa Facebook wa ofisi ya rais. Kinyume na matangazo, ujumbe wa rais haukutangazwa kwenye televisheni ya taifa, anabainisha mwandishi wetu wa Antananarivo, Sarah Tétaud.
Rais wa Madagascar hajatangaza kujiuzulu. “Kuna njia moja tu ya kutatua matatizo haya: kuheshimu Katiba ya sasa ya nchi,” rais wa Madagascar amesema mwanzoni mwa hotuba yake, akifutilia mbali wito wa kujiuzulu lililotolewa na vuguvugu la maandamano la Gen Z. “Tusipofanya hivyo, umaskini utazidi,” ameeleza.
Rajoelina akiwa “mahali salama” baada ya “jaribio la kuua”
Rais wa Jamhuri ya Madagascar pia anadai kwamba, kwa mujibu wa taarifa zake, wanajeshi walikuwa na nia ya kufanya mapinduzi mapema Septemba 25, tarehe ambayo maandamano hayo yalianza, na kujaribu kumuua. “Hii haikunizuia kurejea nchini,” anaongeza Andry Rajoelina, ambaye alikuwa kwenye Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa wakati huo.
Mkuu huyo wa nchi pia amedai kuwa yuko “mahali salama” baada ya kupokea tahadhari inayoonyesha kwamba “watu walikuwa wakijaribu kuniua” katika Ikulu ya Iavoloha. Hata hivyo, hajasema juu ya mahali alipo. Kulingana na RFI, Andry Rajoelina aliondolewa nchini na ndege ya kijeshi ya Ufaransa siku ya Jumapili, Oktoba 12, kwa makubaliano na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron. Rais wa Madagascar aliweza kufika kisiwa cha Réunion kabla ya kusafiri kwa ndege hadi mahali ambapo bado haijulikani kwa wakati huu, akiandamana na familia yake.
Kwa mara nyingine tena amesema kwamba yuko “tayari kwa mazungumzo ili kutatua hali hii.”