Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imeziomba taasisi za elimu zinazotoa mafunzo ya ujasiriamali kwa wanafunzi hususani kupitia mitaala iliyoboreshwa kuzingatia na utoaji wa elimu ya umuhimu wa kodi ili wanafunzi wanapohitimu wawe na maarifa ya kutosha kuhusu wajibu na umuhimu wa ulipaji kodi kwa ajili ya maendeleo ya taifa.
Akizungumza katika maonesho ya ujasiriamali ya wanafunzi wa shule ya kimataifa ya Luminous, Afisa Elimu na Mawasiliano kwa Mlipa Kodi kutoka TRA, Aniceth Ndailagije ameusihi uongozi wa shule hiyo na taasisi nyingine za elimu kuweka mkazo wa somo la kodi kwa wajasiriamali hao wa siku za baadae.
Esterbella Malisa ameandaa taarifa ifuatayo.
Mhariri @moseskwindi