#HABARI: Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bwana Tundu Antipas Lissu inaendelea leo Oktoba 20, 2025 katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam ambapo leo Mawakili wa Jamhuri wakiongozwa na Wakili Mkuu wa Serikali Nassoro Katuga wanajibu mapingamizi ya Lissu aliyeomba Mahakama isipokee ushahidi wa video na flash vilivyowasilishwa na shahidi wa tatu ambaye ni Mkaguzi wa Jeshi la Polisi kutoka Kitengo cha Picha Kamisheni ya Uchunguzi wa Sayansi Jinai Makao Makuu Dar es Salaam, Samweli Kaaya (39) ambaye ameieleza Mahakama Kuu ya Tanzania jinsi alivyofanya uchunguzi wa picha mjongeo na kubaini kuwa picha hiyo ilikuwa halisi na si ya kutengenezwa.

Hoja ya pingamizi kwa mshtakiwa imetokana na maombi ya shahidi ambapo Mkaguzi wa Polisi kutoka Kitengo cha Picha, Kamisheni ya Uchunguzi wa Sayansi Jinai, aliomba kutumia kifaa hicho ili kubaini kama flash disc na memory card alizooneshwa Mahakamani na Wakili wa Serikali Thawabu Issa ni zilezile alizozifanyia kazi wakati wa uchunguzi wake.

•Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *