#HABARI: Wakati vyama vya siasa vikiendelea kukamilisha kampeni zao katika maeneo mbalimbali nchini kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29 mwaka huu, makundi mbalimbali yakiwemo ya kijamii na kidini yameendelea kutoa wito wa kulinda amani. Wameeleza kuwa amani ndiyo tunu kuu ya taifa, hivyo ni wajibu wa kila Mtanzania kuhakikisha inadumishwa kabla, wakati na baada ya uchaguzi.
Mmoja wa wadau wa maendeleo na kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Bwana Manson Kimbo, amesisitiza kuwa vijana wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kulinda amani ya Tanzania kwa wivu mkubwa. Amesema maendeleo ya taifa lolote hutegemea amani, hivyo amewataka vijana na jamii kwa ujumla kuepuka kushiriki katika vitendo vyovyote vinavyoweza kuvuruga utulivu wa nchi, hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.