
Golugwa anakuwa ni kiongozi mkuu wa tatu wa chama hicho kushikiliwa na dola baada ya mwenyekiti Tundu Lissu na makamu mwenyekiti John Heche ambao walikamatwa kwa nyakati tofauti kabla ya uchaguzi.
Viongozi wengine wa chama hicho wanaosakwa ni pamoja na katibu mkuu John Mnyika, na msemaji Brenda Rupia.
Haya yanajiri huku zaidi ya watu 200 nchini Tanzania wameshtakiwa kwa kosa la uhaini siku chache baada ya maandamano ya uchaguzi ambapo upinzani unasema mamia ya watu waliuawa. Haya ni kwa mujibu wa wakili mmoja Peter Kibatala na vyanzo vya mahakama vilivyoliarifu shirika la habari la AFP.